Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Sayyid Mofid Husseini-Kouhsari, katika mahojiano na Shirika la Habari la Hawza, huku akizungumzia mipango ya mabadiliko ya Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza kwa mwaka mpya wa masomo, alisema: “Katika eneo la masuala ya kimataifa, tumeandaa mipango ya mabadiliko kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo, ambayo, Inshaallah kwa fadhila za Mwenyezi Mungu hatua kwa hatua na kwa awamu, tutaanza kuingia katika hatua za utekelezaji wake.”
Kuandaa Sehemu ya Kimataifa kwa Ajili ya Shughuli Zote za Hawza
Alisema kuwa, miongoni mwa mipango ya mabadiliko ni kuandaa sehemu ya kimataifa kwa ajili ya shughuli zote za Hawza za Kiislamu, manaibu, vituo maalumu na mikoa, na kuongeza: “Leo, kuna programu nyingi zinazotekelezwa ndani ya Hawza; kuanzia tamasha hadi programu za utafiti, kisayansi na kielimu, ambazo programu hizi zinaweza kuwa na sehemu ya kimataifa.”
Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza nchini Iran, aliendelea kusema: “Kuweka mwelekeo wa kimataifa katika shughuli na nguzo zote za Hawza, ikiwa ni pamoja na shughuli za kielimu na za utafiti mashuleni, vituo maalumu na mikoa, ni miongoni mwa mipango ya mabadiliko inayofuatiliwa.”
Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Hosseini-Kouhsari alielezea utofauti katika uhubiri katika uwanja wa kimataifa kuwa ni miongoni mwa maeneo mengine ya mabadiliko, na kusema: “Matumizi ya fursa mpya za uhubiri wa mtandaoni katika uwanja wa kimataifa yamewekwa katika ajenda.”
Akirejelea mabadiliko katika uwanja wa mawasiliano na fursa zilizopo katika anga ya mtandao, aliongeza: “Tunajitahidi, kupitia utofauti wa mbinu za uhubiri wa kimataifa na kutumia uwezo wa uhubiri wa kimataifa wa mtandaoni, kuweka mazingira ya mawasiliano yenye ufanisi zaidi na hadhira katika nchi mbalimbali.”
Matumizi Mapana ya Teknolojia za Kisasa na Akili Mnemba
Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza pia aliashiria matumizi mapana ya teknolojia za kisasa na akili mnemba kuwa miongoni mwa maeneo mengine ya mipango ya mabadiliko, na kusema: “Matumizi ya teknolojia za kisasa na akili mnemba katika mawasiliano ya kimataifa, uzalishaji wa kazi za kielimu na za utafiti, tafsiri na uchapishaji wa maudhui ya kielimu, kitamaduni na kidini ya Hawza vimewekwa katika ajenda.”
Aliongeza kwa kusema: “Matumizi mapana ya akili mnemba katika nyanja za elimu, utafiti na uhubiri yanaweza kutoa fursa mpya kwenye shughuli za kimataifa za Hawza.”
Kupanua Ushirikiano kati ya Hawza ya Qum na Najaf
Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Husseini-Kouhsari aliashiria upanuzi wa ushirikiano kati ya Hawza ya Qum na Najaf kuwa ni miongoni mwa maeneo mengine ya mabadiliko, na kusema: “Upanuzi wa mabadilishano ya kielimu na kiutamaduni na Hawza za Kishia na Ahlus-Sunnah katika uwanja wa kimataifa pia unaendelea kufuatiliwa.”
Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza aliendelea kusema: “Kupanua mawasiliano ya kielimu na ya kimadhehebu na taasisi zinazotambulika za kielimu na kimadhehebu pia kumewekwa katika ajenda na kunafuatiliwa kama moja ya mipango ya mabadiliko.”
Kuanzishwa Kituo cha Kimataifa cha Tafakuri kwa Ajili ya Kufuatilia Mabadiliko
Alitangaza pia mipango ya kuanzisha kituo cha kimataifa cha tafakuri, na kusema: “Miongoni mwa maeneo mengine ya mabadiliko ni kuanzisha kituo cha kimataifa cha tafakuri kwa ajili ya kufuatilia, kuchambua na kufanya tafiti za kimkakati katika uwanja wa kimataifa.”
Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza alisisitiza: “Kufuatilia mabadiliko na mageuzi katika uwanja wa kimataifa na kufanya tafiti za kimkakati katika eneo hili ni miongoni mwa programu zitakazofuatiliwa katika mfumo wa mipango ya mabadiliko.”
Kupanua Uendeshaji wa Kozi za Muda Mfupi kwa Wanaopenda Masuala ya Kiislamu Kimataifa
Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Husseini-Kouhsari pia alifafanua upanuzi wa kuendesha kozi za muda mfupi za kuwafahamisha wanaopenda masuala ya kimataifa kuhusu elimu za Kiislamu, na kusema: “Kuna watu walio nje ya nchi, wakiwemo walimu na wasomi mashuhuri, ambao wanapenda kufahamiana na elimu za Kiislamu na elimu za Hawza.”
Aliongeza: “Kupitia kozi za muda mfupi, mazingira ya walimu na wasomi mashuhuri kutoka nje ya nchi kuhudhuria ndani ya nchi yataandaliwa, ili watu hao waweze kushiriki katika programu za kielimu na mafunzo za Hawza.”
Kutoa Mafunzo kwa Wataalamu na Walimu katika Uwanja wa Kimataifa
Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza, akieleza umuhimu wa kutoa mafunzo kwa wataalamu kwa ajili ya kushiriki katika uwanja wa kimataifa, alisema: “Tunajitahidi kuandaa tabaka la wasomi mahiri, pamoja na tabaka la walimu na wataalamu wa Hawza, kwa kuwafahamisha kuhusu uwanja wa kimataifa na suala la lugha.”
Aliendelea kusema: “Lengo ni kwamba, kwa kuandaa tabaka la wataalamu, wachambuzi na wasomi mahiri katika uwanja wa kimataifa, Inshaallah, tuweze kuwa na uwepo na mwingiliano wenye ufanisi zaidi katika matukio ya kielimu.”
Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Husseini-Kouhsari alibainisha: “Kutoa mafunzo kwa wataalamu na walimu katika uwanja wa kimataifa, kuanzia walimu wa ngazi za juu na mafakihi hadi wafasiri, ni miongoni mwa maeneo mengine ya mabadiliko ya kituo hiki.”
Kuanzishwa Mfumo wa Huduma za Kidini za Kimataifa
Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza alielezea kuanzishwa mfumo wa huduma za kidini za kimataifa kuwa ni miongoni mwa programu nyingine za mabadiliko, na kusema: “Kuanzishwa mfumo huu pia kumewekwa katika ajenda, ili mazingira ya utoaji wa huduma za kidini katika uwanja wa kimataifa yaweze kupanuliwa.”
Kuanzishwa Vyama Maalumu vya Pamoja vya Kimataifa
Hujjatul-Islamu wal-Muslimina Husseini-Kouhsari pia alibainisha mipango ya kuanzisha vyama maalumu vya pamoja vya kimataifa, na kuongeza: “Vyama hivi vitaanzishwa kwa kushirikisha walimu na wataalamu wa Iran na wasio Wairani katika nyanja mbalimbali za kielimu na Kiislamu.”
Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza alisisitiza mwishoni: “Mkusanyiko wa hatua hizi unafuatiliwa katika mfumo wa mipango ya mabadiliko ya Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza nchini Iran.”
Maoni yako